Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yusuf Manji ametolewa kwenye Kituo
Kikuu cha Polisi muda mfupi uliopita na kupandishwa kwenye gari la wagonjwa
ambalo lilipita Barabara ya Sokoine kuelekea Posta Mpya.
Mwandishi wa Mwananchi alikuwa eneo
hilo ameshuhudia Manji akipanda gari hilo la Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lakini hawakufahamu mara moja alikoelekea.
Manji alikuwa amevaa fulana, suruali
na viatu vya wazi vyote vya rangi nyeusi.
0 comments:
Post a Comment