Meneja Takwimu Mkoa wa Mara ambaye pia anasimamia timu ya uhamasishaji mkoani hapa, Ramadhani Mbega alisema utafiti huo utafanyika nyumba kwa nyumba maeneo ambayo tayari yametambuliwa.
Utafiti wa aina hiyo ulifanyika mara ya mwisho mwaka 2011/12, mkoa huo ulikuwa na asilimia 4.5 ya maambukizi.
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mara, Dk Nila Jackson alisema uzinduzi wa utafiti huo wa viashiria vya maambukizi ya Ukimwi utasaidia kuwapatia dira na kutambua kiwango cha maambukizi mapya, ili kujua namna ya kuongeza nguvu katika kukabiliana nayo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu watakaofanya utafiti huo.
0 comments:
Post a Comment