Social

Wednesday, March 22, 2017

Kiwango chamtesa Manyika

Manyara. Kiwango kidogo cha kipa namba mbili wa Klabu ya Simba, Peter Manyika imeelezwa kuwa ndiyo sababu ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza katika klabu yake ya Simba.
Kocha wa makipa, Idd Salim Abdallah amesema mchezaji huyo amekuwa chaguo la pili na kushindwa kutumika katika michezo mingi kama si yote ya Ligi Kuu msimu huu hadi sasa na mashindano mengine kutokana na kiwango chake.
Akizungumza jana mjini hapa, Abdallah amesema kipa huyo kinda bado yupo katika katika nafasi nzuri, lakini analazimika kuwa nyuma ya kipa namba moja wa sasa, Daniel Agyei.
Manyika, ambaye alianza kung'ara katika kikosi cha Simba msimu uliopita na kuitwa hadi katika kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars), lakini mambo yanaonekana kubadilika.

0 comments:

Post a Comment