Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba Muhimbili kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu (UNESCO) wamesaini makubaliano ya kuwezesha kutolewa kwa tiba mtandao katika maeneo ya vijijini.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Naibu Makamu Mkuu wa Muhas Profesa Eligious Lyamuya alisema makubaliano hayo yatawezesha madaktari bingwa kuhudumia wagonjwa walio maeneo ya mbali kwa njia ya mtandao.
Amesema kwa kuanzia huduma hiyo itapatikana kwenye kijiji cha Ololosokwani kilichopo wilayani Ngorongoro na imejikita zaidi kwenye tiba inayohusisha masuala ya uzazi na meno.
"Sio lazima daktari bingwa awe kijijini anaweza kuwa mjini na akamtibia mgonjwa akiwa huko aliko, hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo."amesema Profesa Lyamuya








0 comments:
Post a Comment