Iringa. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeifunga benki ya jamii, Mbinga Community Bank Plc, na kusitisha shughuli zake zote za kibenki.
Pia BoT imefuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12 Mei, 2016.
Taarifa iliyotolewa na BoT leo asubuhi, imeeleza kuwa imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe Mei 12 mwaka huu.
Uamuzi huu umechukuliwa baada ya BoT kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.
0 comments:
Post a Comment