Social

Monday, May 29, 2017

Mamia ya waandamanaji wafunga barabara za mitaa Rabat, Morocco


Mamia ya waandamanaji nchini Morocco wamefunga mitaa maarufu katika mji mkuu wa nchi hiyo Rabat, huku maandamano mengine yakiendelea Kaskazini mwa nchi hiyo kwa miezi saba sasa.
Kumekuwa na hali ya wasi wasi tangu siku ya Ijumaa pale vurugu zilipozuka nje ya mji wa al-Hoceima baada ya polisi kujaribu kumshikilia mwanaharakati maarufu Nasser Zefzafi.
Inadaiwa kuwa mwanahakati huyo alivuruga ibada iliyokuwa ikiendelea katika moja ya msikiti.

Nasser Zefzafi ni kiongozi wa maandamano hayo akitaka kuboreshwa kwa hali ya maisha katika mji wa Rif
Image captionNasser Zefzafi ni kiongozi wa maandamano hayo akitaka kuboreshwa kwa hali ya maisha katika mji wa Rif

Vyombo vya habari kutoka nchini humo vinasema kuwa ni nadra vurugu kutokea nchini Morocco.
Hata hivyo hali imekuwa mbaya tangu mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na kisa cha mfanyabiashara maarufu wa samaki al-Hoceima aliyeuawa wakati akiwazuia maofisa wa serikali wasiharibu ghala la samaki wake.

0 comments:

Post a Comment