Social

Friday, May 26, 2017

Ni kwa nini Melania alivaa mavazi meusi akienda Vatican?


Melania Trump aliwasili Vatican akiwa amevalia nadhifu, nguo ndefu, mikono imefunikwa na kujifunika kitambaa cheusi kichwani.
chaguo lake la mavazi hususan kitambaa cheusi, kilitambuliwa sana na wale wanaomfuatilia kwa karibu mama huyo kwa kwanza wakati wa ziara ya kwanza ya mumewe nchi za kigeni.

Bi Trump hakujifunika kichwa alipoenda Saudi ArabiaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBi Trump hakujifunika kichwa alipoenda Saudi Arabia

Kwa kawaida kuna kanuni kali zinazostahili kufuatwa wakati wa kukutana na Papa ambazo White House ilijulishwa.
Kitamaduni viongozi wa nchi na wake zao huchagua kuvaa nguo nyeusi.

Michelle Obama alifunika kichwa akikutana na Papa Benedict XVI mwaka 2009Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMichelle Obama alifunika kichwa akikutana na Papa Benedict XVI mwaka 2009

Watangulizi wake Trump wamefuata kanuni hizo kali. Michelle Obama alichagua kuvaa kitambaa kichwani wakati alimtembelea Papa Benedict mwaka 2009 kama walivyofanya Laura Bush na Hillary Clinton.
Hata hivyo kuna wengine ambao wanapuuza kanuni hizo.

Camilla, hakuvaa nguo nyeusi alipoenda Vatican mwezi Aprili mwaka huuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCamilla, hakuvaa nguo nyeusi alipoenda Vatican mwezi Aprili mwaka huu

Kwa mfano kulitokea malalamiko wakati Cherie Bliar, mke wa aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza alivaa nguo nyeupe mwaka 2006, na pia wakati Camilla, mke wa Prince Charles alivaa suti nyeupe bila hata kujifunika kichwa.
Lakini nchini Saudi Arabia wageni wa kike kutoka nchi za kigeni hawahitajiki kufukina vichwa vyao wakati wanapozuru falme hiyo, isikpokuwa tu wanawake wa Saudia.

White House inasema ilijuliswa kuhusu kanuni za mavaziHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWhite House inasema ilijulishwa kuhusu kanuni za mavazi

0 comments:

Post a Comment