
Guinea. Wafungwa 17 wamepigwa risasi na kuuawa baada ya kuvunja gereza la Buimo, Papua Guinea wakijaribu kutoroka.
Mwaka jana pia wafungwa 12 waliuawa wakijaribu kutoroka katika gereza hilo linalodaiwa kuwa na msongamano wa wafungwa.
Hata hivyo katika jaribio la sasa polisi wamefanikiwa kukamata wafungwa watatu huku wakiendelea kusaka wengine 50.
Inadaiwa kuwa wafungwa hao waliotoroka ni wahalifu sugu.
Idara ya usalama nchini humo imewatahadharisha raia kuwa macho na kuwataka watoe taarifa kwa vyombo vya usalama pindi watakapowaona wafungwa hao.
0 comments:
Post a Comment