Dar es Salaam. Rais John Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki na aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Alosius Mujulizi .
Mujulizi pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania.
Taarifa iliyotumwa na Kitengo cha mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema mwingine aliyeomba kuacha kazi ni Upendo Msuya aliyekuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema katika taarifa hiyo kuwa Rais Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi hao kuanzia Mei 15.
0 comments:
Post a Comment