
Hispania. Mchezaji Fernando Torres (33) amebaki njiapanda baada ya klabu yake kuwa kimya kuhusu mkataba wake unaomalizika mwezi huu Juni.
Mchezaji Saul Niguez aliishauri yake klabu ya Atletico Madrid kumpa mkataba wa kudumu mkongwe Fernando Torres kuitokana na uwezo wake mkubwa uwanjani.
Saul alisema anadhani klabu hiyo inapaswa kumpa mkataba wa kudumu kutokana na kuwa na uzoefu kwenye soka.
"Torres ni mchezaji wa kipekee na yupo karibu na mashabiki bia shaka ameonyesha umuhimu wake kwenye klabu, alinukuliwa Saul alipokuwa akizungumza na gazeti la Marca.
"Ningekuwapo kwenye nafasi ya juu ya uongozi, ningempa mkataba wa kudumu," alisema Saul.
Torres alichomoza akitokea timu ya vijana ya Atletico huku akiwa amecheza mechi 200 za klabu kati ya mwaka 2001 na 7007 kabla ya kuachana na Liverpool.
Pia, aliwahi kuzitumikia Chelsea na AC Milan kabla ya kuamua kurudi kwenye dimba la Vicente Calderon Januari 2015.
Mshabuliaji huyo wa Atletico amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza huku akiwa amefunga mabao 10 kati ya mechi 45 alizocheza katika mashindano yote.
0 comments:
Post a Comment