By Mussa Mwangoka, Mwananchi
Kalambo.
Walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa
kitoweo hicho kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula
nyama hiyo.
Hatua hiyo
imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever
na kuwaacha wengine wakiwa hoi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo
ulijitokeza miezi mitatu iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi na
kusambaa katika kata za Legezamwendo na Mambwe Nkoswe.
Ofisa
Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa alisema nguruwe wote
wanaozagaa mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe.
0 comments:
Post a Comment