By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz
Dare es Salaam. Mwenyekiti wa
Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amewashukuru watu mbalimbali ambao
wamekuwa wakimfariji wakati akiendelea na matibabu ya mguu unaomsumbua.
Akizungumza na gazeti hili jana
nyumbani kwake Mbezi Beach jijini hapa, Mbatia alisema kumekuwa na minong’ono
kuwa anaumwa ugonjwa ambao hautibiki.
Hata hivyo, alisema anaendelea
vizuri na kwamba wakati wowote anaweza kuanza kuendelea na majukumu yake kama
kawaida.
“Mtu akifa watu wanalia na kulalamika
lakini baada ya kuzika kila mtu ananawa mikono na ataelekea anakokujua, lakini
rafiki wa kweli anafahamika wakati wa shida hapo ndiyo unajua kwamba hata siku
usipokuwa dunia watoto, mke na ndugu hao ndiyo watawajulia hali,” alisema
Mbatia.
0 comments:
Post a Comment