Social

Thursday, March 16, 2017

Marufuku mpya ya Trump yazuiwa Marekani


Waandamanaji karibu na White House Machi 11

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine tena, amekumbana na wakati mgumu, katika juhudi zake za kupinga sheria za uhamiaji dhidi ya mataifa yenye Waislamu wengi duniani.
Hii ni baada ya hakimu wa Mahakama Kuu iliyoko Hawaii, kuzuia marufuku hiyo ya Rais, kabla ya kuanza kutumika rasmi.
Amri hiyo kuu ya Rais kwa kiasi fulani, ilikuwa imewazuia wakimbizi na wahamiaji kutoka mataifa kaadhaa kuingia Marekani.
Bwana Trump ameelezea uamuzi huo wa mahakama, kuwa wa kushangaza na ambao haujawahi kufahamika awali, na ameapa kupeleka kesi hiyo hadi katika mahakama ya juu zaidi.

0 comments:

Post a Comment