By Faustine Fabian, Mwananchi
mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Bariadi.
Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge amewaondoa hofu wananchi jimboni mwake kuwa
hakuna atakayefariki dunia kwa njaa kwa sababu vipo vyakula vya kutosha.
Chenge
alitoa kauli hiyo katika Kijiji cha Mwantimba Kata ya Matongo mkoani Simiyu
baada ya wakazi hao kumwomba awapatie mahindi ya msaada ili kukabiliana na njaa
inayowanyemelea.
Ofisa
Mtendaji wa kijiji hicho, Kija Thelathini alimweleza mbunge huyo kuwa wananchi
hulazimika kula mlo mmoja kwa sababu mazao waliyopanda yamekauka.
Mwenyekiti
wa CCM wilayani humo, Juliana Mahongo alimtaka mbunge huyo kufikisha kilio chao
katika mamlaka husika ili wapelekewe mahindi ya msaada watakayouziwa kwa bei
nafuu.
0 comments:
Post a Comment