By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.Tz
Dar es
Salaam. Asilimia 69 ya Watanzania wanakabiliwa na uhaba wa chakula
tangu mwakan2016, utafiti umeeleza.
Matokeo ya
utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza Februari yanaonyesha kuwa asilimia 51
ya kaya hazikuwa na Chakula chankutosha au mwanakaya ameshinda njaa kwa sababu
hakuweza kupata Chakula.
Akifafanua
kuhusu utafiti huo leo Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze
alisema takwimu zake zimekusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,800 wa Tanzania Bars
kati ya Septemba 14-26, 2016 nabkutoka kwa wahojiwa 1,610 kati ya February
9-15, 2017.
"Kwa
mujibu wa wananchi wengi, Uhakika wa kupata chakula umepungua kati ya Septemba
2016 na February 2017. Asilimia 65 ya wananchi walikuwa na hofu ya Maya
zaobkukosa chakula cha kutosha ikilinganishwa na asilimia 45 waliosema hiyo
Septemba 2016," alisema Eyakuze.
"February
2017 asilimia 51 ya wananchi waliripoti kwamba kuna wakati hawakuwa na Chakula
ch kutosha kwa ajili ya kaya zao katika kipindi cha miezi mitatu
iliyopita," aliongeza.
0 comments:
Post a Comment