Social

Monday, March 20, 2017

TCAA yaburutwa kortini


Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa zabuni ya ufungaji wa rada katika viwanja vinne vya ndege nchini iko njia panda baada ya kampuni ya Geci Espaniola S.A kutoka Hispania kuishtaki Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ikidai kuna ukiukwaji wa sheria katika kumpata mzabuni.
Kampuni hiyo iliyokuwa miongoni mwa wazabuni imekata rufaa katika Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA), ikipinga hatua ya TCAA kuiengua katika zabuni.
Kwa mujibu wa hati ya rufaa ya kampuni hiyo, katika zabuni Geci ilitoa ofa ya Dola 18.8 milioni za Marekani na Sh1.3 bilioni, ikiahidi kutumia teknolojia ya kisasa. Zabuni hiyo ilitangazwa na TCAA Septemba 2016 kwa ajili ya kusambaza na kufunga rada na vifaa vya usalama katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (Kia), Mwanza na Songwe.
Inadai TCAA iliiengua na kutoa zabuni kwa kampuni ya Thailes Air System ya Ufaransa kwa gharama ya Euro 22,351,248 na Sh3.671 bilioni ambayo ni kubwa. 

0 comments:

Post a Comment