Dar es
Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliani, Profesa Makame
Mbarawa amezindua rasmi huduma ya kuhama mtandao (MNP) na kuwaonya watoa huduma
(mitandao) watakaowakwamisha wateja wao kuhama.
Profesa
Mbarawa amesema huduma hiyo imeanzishwa ili kumpa uhuru mtumiaji wa kuchagua
huduma bora, jambo litakalowafanya watoa huduma kuboresha huduma zao.
Amesisitiza
kwamba matumizi ya mfumo wa MNP yatafanikiwa kwa sababu ni rahisi ukilinganisha
na ule wa kuhama kutoka analogi kwenda digitali uliofanyika miaka michache iliyopita
na kuipa sifa Tanzania.
"Tunataka
wananchi wajue kwamba huduma hii ni bure na wasilazimishwe kuhamia mtandao
fulani kwa kushinikizwa. Hii ni Huduma ya hiari na hatutasita kuchukua hatua
kwa kampuni ya simu itakayokiuka utaratibu huu," amesema.
Huduma hii
ya MNP katika Afrika inatumika katika nchi nane, lakini kwa Afrika Mashariki
inapatikana Kenya pekee na Tanzania leo inakuwa ya pili wakati nchi za Rwanda
na Uganda wakiwa kwenye mchakato huo.
0 comments:
Post a Comment