By Joseph Lyimo, Mwananchi
jlyimo@mwananchi.co.tz
Simanjiro.Mifugo
zaidi ya 4,000 ya wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imekufa kwa
kukosa maji na malisho kutokana na ukame ulioikumba wilaya hiyo.
Wakizungumza
juzi kuhusiana na tatizo hilo, wafugaji hao walidai kuwa ukame uliozikumba
sehemu mbalimbali wilayani humo umesababisha mifugo yao ikiwamo ng’ombe, mbuzi
na punda kufa.
Alex
Mollel mmoja kati ya wafugaji hao alisema yeye binafsi amepoteza zaidi ya
ng’ombe 250 kutokana na ukame na wafugaji wengi pia wamepata hasara kutokana na
ukame huo ambao haujawahi kutokea.
“Huu ukame
wa kipindi hiki umetusababishia hata bwawa la Kidawashi kukauka na pia
mifugo imekosa maji na malisho hali inayosababisha hasara kubwa kwa wafugaji
wengi,” alisema Mollel.
Alice
Laizer alisema wingi wa mifugo umesaidia wafugaji wengine kubaki na baadhi ya
mifugo baada ya mingine kufa, kwani endapo wangekuwa na mifugo michache, wengi
wao wangeishiwa mifugo yote.
“Mfano
kina Orenji walikuwa na ng’ombe 2,500 na hao 500 wakafa hivyo wamebaki ngombe
2,000 na baada ya miaka miwili au mitatu hiyo iliyobaki itazaana na kurudia
idadi ya awali,” alisema Laizer.
0 comments:
Post a Comment