Marekani, Uingereza na nchi
nyengine katika Baraza la Usalama, zilitaka kuiadhibu Damascus kwa tuhuma za
kutumia silaha za sumu katika maeneo ya waasi.
Ni mara ya saba sasa Urusi
inatumia kura yake ya VETO kuikinga serikali ya Rais Assad na tuhuma za kimataifa.
Katika hotuba yake iliyojawa
hisia kabla ya kura, balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Matthew
Rycroft, alisimulia kifo cha mwathirika mmoja ambae alipelekwa katika hospitali
baada ya shambulio la gesi yenye sumu.
Hata hivyo, kwa upande wake,
balozi wa China katika Umoja wa Mataifa, Liu Jieyi, ameliambia Baraza la
Usalama kwamba bado hakuna vilelezo kwamba serikali ya Syria imetumia silaha za
kemikali.
Naye Rais Vladmir Putin amesema
vikwazo vitazuia jitihada za mazungumzo ya amani yanayoendelea Geneva baina ya
serikali na wapinzani wake.
Marekani imesema Urusi na China
zimekataa kuwajibisha vikosi ambavyo viliangusha gesi za sumu na kusababisha
vifo vya wanaume, wanawake na watoto.
0 comments:
Post a Comment