Madrid, Hispania.Ronaldinho amesema anaamini Neymar amefikia viwango vya mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi na nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo. Neymar amekuwa na muunganiko mzuri na wachezaji wenzake wa Barcelona, Luis Suarez na Messi ameendelea kuiteka dunia kutokana na kiwango chake anachokionyesha kwa sasa Barcelona.
Neymar (25) amefanikiwa kushinda mataji mawili ya La Liga na moja la Ligi ya Mabingwa na kuibuka kuwa kinara miongoni mwa wachezaji barani Ulaya.
Ronaldinho ambaye amewahi kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) alisema, "kwa sasa Neymar amefikia kiwango cha kuwa mchezaji bora na unaweza kumliganisha na Ronaldo na Messi."
"Neymar ni rafiki yangu wa karibu na kwa sasa ni mchezaji maarufu nchini Brazil" alisema Ronaldinho alipokuwa Dubai juzi wakati akizungumza na Mtandao wa Gulf.
Kama ilivyo kwa Neymar, pia Ronaldinho aliipa mafanikio makubwa Barcelona kwa kuiwezesha kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2006.
Hata hivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alisema asingependelea kuilinganisha timu yake ya zamani na Barcelona ya sasa.
"Sipendi kuifananisha timu ya zamani ya sasa. Hii ni timu kubwa yenye wachezaji bora na hata hivi sasa imeendelea kuwa timu bora yenye wachezaji bora," alisema Ronaldinho.
"Ninafurahia mafanikio yangu na timu. Tulishinda mataji mengi na hata Barca ya sasa inafanya vyema na wamepata mafaniko makubwa. Ninawatakia mafanikio zaidi. Isipokuwa sipendi kufananisha mambo ya zamani na sasa. Ninachofahamu timu imeendelea kufanya vyema."
0 comments:
Post a Comment