Dar es Salaam. Lori la kubeba mafuta la kampuni ya Petro limeungua moto wakati likishusha mafuta katika sheli ya Petro, Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Manispaa ya Ilala, Elinimo Shang’a alisema chanzo cha moto huo ni hitilafu iliyojitokeza baada ya kukanyagwa kwa nyaya ya umeme.
“Baada ya nyaya hiyo kupata hitilafu, moto ulishika katika ndoo ya mafuta ya petrol iliyokuwa karibu na eneo hilo na kudaka kwenye lori hilo la mafuta,” alisema Shang’a
Meneja wa Sheli hiyo, Naila Khamisi, alisema kwa sasa hawezi kujua moto huo umeleta madhara kiasi gani hadi watakapofanya tathmini.
“Nashukuru jeshi la zima moto ambao wameweza kuonyesha ushrikiano wa kuweza kuzima moto huo.” Alisema Khamis
0 comments:
Post a Comment