Social

Tuesday, March 7, 2017

Arsenal yamtia kiwewe Ancelotti



London, England.Carlo Ancelotti bado anasumbuliwa na kumbukumbu mbaya katika michezo ya Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo bosi huyo wa Bayern Munich anamini timu yake haitoruhusu ushindi wao mabao 5-1 kupinduliwa na Arsenal  leo usiku.
Ancelotti alikuwa kocha wakati AC Milan ilipotolewa kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4 na Deportivo La Coruna baada ya kushinda katika mchezo wa kwanza wa robo fainali 4-1 mwaka 2004.
Pia, hali hiyo ilijitokeza 2005, katika fainali ya Istanbul, wakati Liverpool iliposawazisha kutoka 3-0  kipindi cha kwanza kumaliza mechi 3-3 kabla ya kushinda kwa penalti.
“Nataka kusahau kabisa michezo hiyo, lakini sitotaka ijirudie,” alikiri Ancelotti. “Sasa nafikiri kuwa uzoefu huo ni mzuri kwangu kwa sababu itanisaidia katika mchezo huo.
“Tumejiweka katika mazingira mazuri  baada ya mchezo wa kwanza nyumbani Munich na hiyo ni habari njema kwetu kuonyesha uwezo wetu kwa kuhakikisha tunashinda na kusonga mbele.
“Nitaanzisha kikosi bora kwa sababu najua ubora wa Arsenal watakuja kutushambulia kuanzia mwanzo wakijaribu kupata bao la mapema.
“Najua kuwa Arsenal wamekuwa wakilaumiwa na mechi hii itakuwa muhimu kwao katika kuhakikisha wanatatua matatizo yao.

0 comments:

Post a Comment