Social

Tuesday, March 14, 2017

Kocha Conte akiponda Man United



Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji alijikuta akichezewa vibaya kutokana na makali aliyokuwa akiyaonyesha kwenye mchezo huo. Kutokana na mchezo kuwa wa nguvu na rafu nyingi, ilisababisha Ander Herrera kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kufikisha jumla ya kadi mbili za njano.
Baada ya Chelsea kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United, Kocha Conte alisema, "Katika dakika ya 20, 25 ilikuwa ni vigumu kwa Hazard kucheza mpira. Niliona alipata nafasi nyingi. Sidhani kama mimi ni mjinga niliona yote aliyokuwa akiyafanya."
Kwa matokeo hayo Chelsea imesonga mbele katika hatua ya nusu fainali na itakutana na Tottenham huku Arsenal itakwaana na Manchester City.
"Alikuwa akipata mipira mingi lakini hakuifanyaia kazi. Hakuna mtu ambaye hakuona jambo hilo."
Wakati Jose Mourinho alipokuwa kocha wa Chelsea aliwahi kulaumiwa kutokana na kutofanya jambo la maana katika michezo 10 ambayo timu ilikuwa imecheza. Lakini Conte amefanikiwa kukisuka upya kikosi hicho na kumfunika bosi huyo wa zamani wa Chelsea kutokana na kuwa na mbinu nyingi zaidi.
Kocha huyo raia wa Italia alisema, "Mbinu hii ya kucheza kwa kushambulia na kuzuia  haiwezi kutusaidia. Sipendelei aina hiyo ya soka na wala mbinu hiyo haiwezi kutusaidia."
"Wakati mwingine nafikiria kwamba  wakati unapokutana na wachezaji wengi wenye uzoefu na vipaji unaweza kujitahidi kuwasoma wachezaji hawa. Nafikiri mwamuzi anatakiwa kuwalinda  aina hii ya wechaji."
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho alisifu kikosi chake akisema kwambam "Timu yangu ilicheza vizuri lakini mchezo ni dakika 90. Kutolewa mchezaji wetu kwa kadi nyekundu kulitutoa mchezon."
Mourihno alisema kwamba licha ya kupoteza mchezo huo muhimu sasa kikosi chke kinapaswa kuelekeza nguvu kwenye mchezo wao na Rastov kwenye robo fainali ya Ligi ya Europa mechi itakayopigwa kesho.

0 comments:

Post a Comment