Social

Tuesday, March 14, 2017

Cafu: Neymar atampiku Pele



Sao Paolo, Brazil.Beki wa zamani wa Brazil, Cafu anaamini Neymar  ataivunja rekodi ya Pele ya kufunga mabao mengo katika timu ya taifa.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona amefunga mabao 50 katika timu ya taifa akizidiwa na Pele, Ronaldo na Romario waliofunga zaidi yake.
Pele ameifungia Brazil 'Selecao' mabao 77, lakini Cafu anaamini Neymar ataivunja rekodi hiyo kwa sababu ya umri wake na kipaji chake.
Cafu aliimbia Fifa: "Rekodi zote zipo kwa ajili ya kuvunjwa. Naamini Neymar ataivunja rekodi hiyo.
"Bado ni kijana kama ataendelea kucheza kwa kiwango cha sasa, kuna uwezekano mkubwa ya kuivunja rekodi ya Pele."
Neymar amefunga mabao manne katika mechi tano zilizopita pia ameiongoza nchi yake kutwaa medali ya dhahabu ya Michezo ya Olimpiki 2016.

0 comments:

Post a Comment