Social

Tuesday, March 14, 2017

Diamond Platnumz avitaka vyombo vya habari kuacha kukuza mgogoro ambao haupo kati yake na Ali Kiba




Mwanamuziki Diamond Platnumz ametangaza rasmi leo kuwa hana mgogoro wowote na Alikiba huku akivitaka vyombo vya habari kuacha kuzusha habari za kuwa wao wawili hawaelewani.

Hitmaker huyo wa Marry You amesema hayo Jumanne hii wakati alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV.

Mimi nimefahamiana na Ali tangu hata sijatoka, ule wimbo wake wa matonge (Usiniseme) mimi ndio nilimpa wale 'dancers' nikamwambia watafanya kiti kizuri. Wakati mimi ndio naanza muziki nilikuwa nikimpigia simu kumuomba msaada, na hata safari yangu ya kwanza kwenda Uingereza, nilikuwa nikimuuliza jinsi ya kujaza fomu ya kuomba visa, alisema Diamond Platnumz.

Alipoulizwa kama amewahi kukutana na Ali siku za karibu, Diamond Platnumz alisema kuwa, walikutana na Alikiba Nairobi ambapo walikaa na kuzungumza mambo yanayowahusu wao. Kuhusu kuweka nyimbo za Alikiba kwenye tovuti yake, Platnumz alisema hana tatizo juu ya hilo kwani hiyo ndiyo itakuwa njia salama zaidi kama nyimbo za wasanii wote zitakuwa pamoja.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Diamond Platnumz ameandika na kuvisihi vyombo vya habari kuacha kukuza mgogoro ambao haupo kati yake na Ali.

The post Diamond Platnumz avitaka vyombo vya habari kuacha kukuza mgogoro ambao haupo kati yake na Ali Kiba appeared first on Zanzibar24.
Zanzibar 24 

0 comments:

Post a Comment