Social

Sunday, March 26, 2017

Kigogo Tume ya Utawala Bora aonya viongozi



Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Tom Nyanduga ameonya dhidi ya vitendo alivyoviita havifuati utawala wa sheria, akisema vitasababisha wananchi kupoteza imani.
Akizungumza katika kipindi cha Kipima Joto kilichorushwa juzi usiku na kituo cha televisheni cha ITV, Kamishna Nyanduga alisema kitendo cha kiongozi kuonyesha upendeleo katika uwajibikaji, kinapoteza imani kwa wananchi.
"Sidhani kama ukiwa kiongozi unakuwa na mamlaka yasiyo na mipaka, (au) utafanya mambo yote bila kushauriwa. Dhana ya uwajibikaji ni muhimu sana katika uongozi bora," alisema bila ya kutaja upendeleo gani.
"Isiwe kuwajibishwa na mamlaka iliyo juu yako, lakini ule ukomo wa madaraka ulionao ukufanye wewe mwenyewe ujisahihishe," alisema Nyanduga.
"Athari zake kwanza ni upotevu wa imani, tunaweza tusiwe na kigezo cha kupima. Upotevu wa imani ni kitu ambacho unaweza usikishike, lakini unaweza kuhisi upotevu wa imani unatokea kutokana na matendo au matamko ambayo hulka ya viongozi ambayo inakuwepo kipindi hiki."
Alitoa mfano wa enzi za utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akisema wakati nchi inapitia kipindi kigumu, Mwalimu alieleza hali ilivyokuwa na mikakati ya Serikali hivyo kuwajengea imani wananchi.


0 comments:

Post a Comment