Social

Wednesday, March 22, 2017

Hesabu zimeshakataa Msuva kufauata nyayo za samatta




Itakuja Oktoba 2, mwaka huu kama Mungu akimpa pumzi. Wakati huo, mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta atakuwa bado ana miaka 24. Miezi miwili baada ya hapo Samatta ndio atakuwa ametimiza miaka 25. Hii ina maana kuwa Samatta na Msuva hawajapishana sana kiumri.
Ukimaliza hesabu hizo anza kujiuliza Samatta aliondoka lini nchini. Inaonyesha kuwa aliondoka mwaka 2011. Hii ni miaka sita iliyopita. Miaka mitano ameitumia akiichezea klabu ya TP Mazembe ambao ni wababe wa Afrika.
Ndani ya miaka hii sita, Samatta amekomaa kiuchezaji. Alicheza fainali ya Afrika. Alicheza hatua nyingi za juu katika michuano ya Afrika. Alicheza hadi michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Na sasa ana mwaka mmoja Ulaya.
Ndani ya mwaka mmoja huu Ulaya, Samatta ndio anaanza kuzoea na kutangaza jina lake. Anajitahidi kupigana. Anafunga mabao mengi kwa sasa. Ikifika Juni mwaka huu ndio tutajua kama atapata timu kubwa zaidi ya Genk. Inawezekana Mungu akamjalia akaenda juu zaidi.
Kama safari ya Samatta inaweza kumfisha katika timu kubwa zaidi Ulaya, basi atakuwa na miaka 28 hivi. Hii ina maana kwa sasa anaweza kwenda katika timu kama Bayer Leverkusen au Borussia Dortmund. Aking'ara huko kwa miaka miwili hivi au mitatu atakuwa na miaka 28. Hapo anaweza kwenda timu zaidi ya hizo, ambazo ndizo tunazishabikia Ulaya.
Safari yake ilichelewa na alikaa miaka mitano Mazembe akipata uzoefu. Leo Msuva bado yupo Yanga na ana miaka 23. Anahitaji bahati ya mtende sana kuweza kufika timu kama Genk ghafla na kuachana na njia aliyotumia Samatta kwenda Mazembe kabla ya kuibukia Ulaya.
NILIKUWA napitia tena tarehe za kuzaliwa wachezaji wetu. Nikapitia jina la Simon Msuva. Ndiye mchezaji anayeibeba Yanga kwa sasa. Alizaliwa Oktoba 2, 1993. Kwa sasa ana umri wa miaka 23. Ukisikia kuna sherehe nyingine ya kuzaliwa kwa Msuva basi atakuwa ametimiza miaka 24.
Katika akili ya kawaida itakuwa vigumu kwa Msuva kupata mafanikio Ulaya kwa sasa. Farid Mussa amelishtukia hili mapema na akiwa na miaka 20 tayari yupo Ulaya, hata kama yupo katika timu ya daraja la kwanza. Ndani ya miaka mitatu ya kula vizuri, kulala vizuri na kufundishwa vizuri anaweza kuwa mbali na wakati huo atakuwa na miaka 23 tu.
Kitu cha msingi kwa Msuva kwa sasa ni kuhakikisha kuwa Yanga inamlipa vizuri zaidi. Yeye ndiye mchezaji muhimu zaidi katika kikosi chao kwa sasa. Mabao mengi zaidi yanapitia kwake kwake kwa sasa. Anajituma sana na amepigana kujipatia heshima yake Yanga.
Sioni uwezekano wowote wa Msuva kuondoka Yanga kabla hajatimiza miaka 24 Oktoba 2 , mwaka huu. Na kwa sababu hilo halipo kwa sasa basi anachoweza kukifanya kwa sasa ni kujaribu kuyajenga maisha yake kupitia Yanga.
Kuna wachezaji wengi wa kigeni pale Yanga wanachukua pesa nyingi, tena kwa dola, kuliko yeye wakati mchango wao unaweza kuwa mdogo au sawa na wake. Inawezekana hajitambui sana au hana mtu wa kumsimamia ndio maana anachukulia kawaida tu.
Afanye kila anachoweza ajitambue kwa sasa na alipwe chake vizuri. Vinginevyo sioni kama Msuva anaweza kuifuata safari ya Samatta wakati Oktoba 2 anatimiza miaka 24 na bado anakipiga Uwanja wa Taifa.

0 comments:

Post a Comment