Brazil itaivaa Ujerumani mwakani kwa mara ya kwanza tangu waliponyukwa kwa mabao 7-1 katika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Timu hizo mbili za taifa mashuhuri zaidi duniani zitarudiana kwenye Uwanja wa Olympic, Berlin mwezi Machi 27, 2018.
Kocha Tite ameifanyia mabadiliko makubwa kikosi cha Brazil tangu nchi hiyo ilipopata kipigo kikubwa zaidi katika historia.
Katika wiki chache zijazo inaweza kuwa timu ya kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.
Kocha huyo wa zamani wa Corinthians anataka Brazil icheze na wapinzani wake wakubwa kabla ya fainali ya Russia.
Kwa hiyo baada ya kupanga tarehe dhidi ya Ujerumani, Tite sasa anaangalia uwezekano wa kupata mechi dhidi ya Italia na Hispania.
0 comments:
Post a Comment