
London, England .Steven Gerrard amesema Liverpool wanatakiwa kuvunja benki na kumsajili mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang mwisho wa msimu.
Kocha Liverpool, Jurgen Klopp yupo katika harakati za kutafuta mshambuliaji bora duniani katika jitihada zake za kutegeneza kikosi bora kitakachowasaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Gerrard anaamini nyota wa Borussia Dortmund, Aubameyang ndiye mchezaji sahihi anayemfaa Klopp kama anataka kumalisha kikosi chake.
Alipoulizwa na mchambuzi mwenzake wa BT Sport, Gary Lineker kama Aubameyang ndiye mchezaji anayestahili kuichezea Liverpool, alijibu: "Yeah, kwa sababu aina yake ya uchezaji inazivutia klabu nyingi si Liverpool pekee.
Gerrard alisema Aubameyang ni mchezaji wa aina inayotakiwa na Liverpool.
"Ushambuliaji wake ni hatari kila wakati anapokuwa na mpira na jinsi anavyoweza kubadilika kwa haraka."
Aubameyang kwa sasa anaongoza kwa ufungaji katika Ligi ya Ujerumani baada ya kufunga mabao 21 katika michezo 21 alizocheza.
0 comments:
Post a Comment