Hispania.Kocha Diego Simieno wa Atletico, Madrid amejifariji na suruhu aliyopata juzi na kuwawezesha kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Alisema akili yake ameielekeza kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo dhidi ya Sevilla inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo.
Atletico Madrid ilikata tiketi ya kutinga kwenye mashindano hayo, huku wakipenya kwenye hatua hiyo kwa kuiondoa Bayern Leverkusen kwa jumla ya mabao 4-2.
Bayern Munich, Juventus, Barcelona, Real Madrid, Borussia Dortmund, Monaco, Leicester City na Atletico Madrid ndizo zilizotinga kwenye hatua ya robo fainali.
Simione amesema kwamba timu hizo hazimuumizi kichwa kwani akili yake ameilekeza kwenye mechi ya keshokutwa dhidi ya Sevilla katika La Liga.
"Kinachoniumiza kichwa ni mechi ya wiki hii dhidi ya Sevilla," alisema Simieno
"Timu yangu haijaathirika licha ya kutoka droo, timu yoyote tutakayopangiwa tutakabiliana nayo. Hii ni hatua muhimu tuliyofikia lakini ni hatua moja. Ligi ya Mabingwa siku zote ni kitu muhimu na hili ni jambo muhimu kwa klabu," aliongeza.
Anasema, "Ninapenda kushukuru juhudi kubwa zilizofanywa na klabu hii hususan wachezaji ambao wameonyesha kujituma kwa kila namna ndani ya kipndi hiki cha miaka minne."
0 comments:
Post a Comment