Social

Wednesday, May 3, 2017

Hispania: Neymar awaita Manchester United mezani


Barcelona, Hispania. Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar, 25, amewaambia rafiki zake kuwa Manchester United inataka kuvunja rekodi ya uhamisho wa dunia kwa kul
ipa kiasi cha Pauni 170 milioni, ambacho kinamruhusu katika mkataba wake kuondoka Barcelona.
Inadaiwa kuwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amekuwa akimfuatilia Neymar kimya kimya na amemwambia staa huyo wa kimataifa wa Brazil kuwa Manchester United ipo tayari kununua mkataba wake na kumlipa mshahara zaidi ya anaolipwa sasa.

Mourinho anatazamiwa kuanza Ligi Kuu ya England msimu ujao bila ya Wayne Rooney anayetazamiwa kuondoka mwishoni mwa msimu na pia bila ya Zlatan Ibrahimovic, ambaye hata akipewa mkataba mpya bado ana matatizo ya goti.

0 comments:

Post a Comment