Social

Wednesday, May 3, 2017

London: Liverpool yamtaka Douglas Costa



London. Taarifa zinadai kuwa Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametenga kiasi cha Pauni 26 milioni kwa ajili ya winga wa Bayern Munich, Douglas Costa.
Hata hivyo rafiki wa karibu wa winga huyo, Lucas Cruel, ambaye pia ni kocha wake binafsi amedai kuwa hakuna nafasi ya Costa kwenda Liverpool.
Staa huyo wa kimtaifa wa Brazil ameelezea nia yake ya kuondoka Allianz Arena mwishoni mwa msimu huu baada ya nafasi yake kuwa ndogo klabuni hapo chini ya kocha Carlo Ancelotti.

0 comments:

Post a Comment