Social

Tuesday, March 21, 2017

Wimbo wa Ligi ya Mabingwa wamliza kocha wa Atletico Madrid



Hispania. Uchungu kwa Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone baada ya kutolewa kwenye kinyang'anyiro cha kuingia Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, umekolezwa na wimbo ambao huwa unawekwa kama ishara kabla na wakati wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Atletico walipoteza imekuwa na bahati kilka mara kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na walipoteza kwa penalti walipokutana na Real Madrid msimu wa 2015-16 katika mchezo wa fainali katika mashindano hayo uliopigwa mjini Milan, Italia.
Timu hiyo imepoteza michezo yake katika misimu mitatu dhidi ya Real Madrid kwenye hatua ya fainali, huku ikiondolewa  kwa kuchapwa mabao 4-1 mjini Lisbon jambo lililoweka rehani kibarua cha kocha wao Simeone.
"Kila wakati ninaposikia ule wimbo unaoashiria mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya najisikia vibaya," amesema Kocha Simione.

0 comments:

Post a Comment