Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), leo inawapa mafunzo mbalimbali wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya miundombinu ili kuwajengea uwezo wabunge hao.
Miongoni mwa maeneo watakayofundishwa wabunge hao ni masuala yanayohusu vyanzo vya mapato Serikalini, anuani ya makazi na masuala ya mtandao na matatizo yake.
Akizungumza na wanahabari kabla ya kuanza mafunzo hayo yaliyofanyika makao makuu ya TCRA, mwenyekiti wa bodi wa mamlaka hiyo, Jones Kilembe amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo ili wabunge hao wajue shuguli zinazofanywa na chombo hicho.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla amesema wajumbe wa kamati yake wataelimika zaidi na kupata ujuzi wa kujua namna gani wataweza kuisimamia Serikali kwenye sekta hiyo.
0 comments:
Post a Comment