MONACO, UFARANSA.KOCHA WA MACHESTER CITY, PEP GUARDIOLA AMESEMA MCHEZO USIOVUTIO ULIOONYESHWA NA KIKOSI CHAKE KATIKA KIPINDI CHA KWANZA NDIYO SABABU YA KUTOLEWA KATIKA MASHINDANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA BAADA YA KULAZWA MABAO 3-1 DHIDI YA MONACO.
Manchester City katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo iliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-3.
"Kipindi cha pili tulicheza vizuri, lakini tulizinduka tayari wenzetu wakiwa wamejimarisha," alisema Guardiola alipokuwa akizungumza na BT Sport.
"Tulikuwa na nafasi nzuri kutokana na mchezo wa awali kushinda, tulicheza vyema kipindi cha pili na tukajisahau kuzuia mabao."
"Hicho kilichotokea tumejifunza. Tumeingia kwenye mashindano haya na kikosi ambacho hakina uzoefu wa kutosha. Kipindi cha pili tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda mabao mengi. Lakini hatukufanya hivyo na ndiyo maana tumetolewa."
"Wakati wingine historia inaweza kukuhukumu. Hatukuwa kwenye kiwango kizuri kimchezo. Tutahakikisha tunajiimarisha lakini katika mchezo wakati mwingine unaweza kubebwa na bahati. Hivyo sisi hatukuwa na bahati."
0 comments:
Post a Comment