Tabora. Baada ya uamuzi wa kutengua nyadhifa za watendaji wa Bodi ya Chama Kikuu cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (Wetcu Ltd), siri ya hatua hiyo imefichuka.
Hatua hiyo imeelezwa ni kutokana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku, Wilfred Mushi kutumia muda kusafiri kwenda Morogoro na jijini Dar es Salaam badala ya kushughulikia masuala ya wakulima.
Jana, Waziri Mkuu alitoa uamuzi wa kuwatimua mkurugenzi huyo na mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku, Vita Kawawa kwa kushindwa kuwajibika.
Uongozi huo pia unadaiwa kufanya udanganyifu katika mauzo ya hisa za ushirika katika Benki ya CRDB na kutoa taarifa za uwongo kwa wanachama.
Katika mlolongo wa tuhuma hizo, mwenyekiti na makamu wake wanadaiwa kujilipa posho mbalimbali zinazofikia Sh23 milioni kila mmoja.
Ukarabati wa majengo ya shirika hilo pia unadaiwa kugubikwa na utata baada ya kugharimu Sh170 milioni badala ya Sh33 milioni zilizotengwa.
0 comments:
Post a Comment