Social

Tuesday, March 7, 2017

Simba yatupwa kwa Madini FA


Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza ratiba ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) huku Simba ikipangwa kucheza Madini ya Arusha Machi 18.
Ratiba hiyo inaonyesha michezo mingine itakuwa Kagera Sugar dhidi ya Stand United, Azam FC itachuana na Ndanda kwenye Uwanja wa Azam Complex na mshindi wa mchezo kati ya Yanga na Kiluvya United atakumbana na wajerajera Tanzania Prisons.
Mchezo baina ya Madini na Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha utavuta hisia za wapenzi wa soka wa mkoa huo na mikoa mingine ya jirani watakaotaka kuishudia Simba kwa Mara ya kwanza baada ya kupita miaka minne.
Mshindi wa Kombe hili atajinyakulia kitita cha Sh. 50 milioni na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

0 comments:

Post a Comment