Social

Tuesday, March 7, 2017

Ronaldo, Bale kuivaa Napoli



Roma, Italia.Cristia o Ronaldo na Gareth Bale wamejumuhishwa katika kikosi cha Real Madrid kitakachoanza leo dhidi ya Napoli katika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Wawili hao waliukosa mchezo wa Jumamosi ambao Real ilishinda 4-1 dhidi ya Eibar katika Ligi Kuu Hispania.
Ronaldo amepona majeruhi yake na mwenzake Bale alikuwa akitumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja.
Beki wa kati Raphael Varane ataikosa mechi hiyo kutokana na kusumbuliwa ana majeruhi.
Napoli ilifungwa 3-1 katika mchezo wa kwanza, wameimalika zaidi baada ya kurejea kwa winga wake Dries Mertens aliyekuwa akisumbuliwa na majeruhi.
Mertens alifunga mabao wakishinda 2-1 dhidi ya Roma katika Serie A , wakati Roma itambikiwa na Napoli.

0 comments:

Post a Comment