Social

Friday, March 17, 2017

Maeneo saba Mwanza kupata maji



Ilemela. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Mwanza (Mwauwasa), Antony Sanga amesema maeneo kadhaa katika mikoa ya Simiyu na Mwanza yatanufaika na uwezeshaji wa kifedha kutoka taasisi mbili za kimataifa.
Hata hivyo, Sanga ambaye amezungumza na mwandishi wa habari hii mjini Mwanza ametaja maeneo yaliyopo jijini humo pekee kuwa ni ni Nyasaka, Bugarika, Nyegezi, Capripoint, Mjimwema, Nyakabungo na Kitangiri.
 Amesema Serikali nchini kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) wanatarajia kutumia Sh245 bilioni kwa ajili ya mradi wa maji kwenye miji sita ya mikoa ya Mwanza na  Simiyu.
 Sanga ametoa ufafanuzi huo baada ya wakazi wa mitaa miwili ya Kahama na Magaka iliyopo katika Wilaya ya Ilemema mkoani Mwanza kulalamika kuwa wametengwa na Serikali kiasi cha kulazimika kutembea umbali wa kilomita tano kwenda kukesha wakisubiri maji ya visimani.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Magaka, George Mwakaponda amesema kuwa walishapeleka maombi serikalini ili tatizo la maji katika eneo hilo lishughulikiwe, lakini mamla za umma hazijafanya lolote kuwaondolea kero hiyo.
 Mwakaponda amesema kilio hicho cha wananchi kimekuwa ni cha muda mrefu na kwamba, wako radhi wapate huduma ya maji kuliko umeme ambao wanauchukulia kuwa anasa, lakini maji ni huduma muhimu kwa maisha yao.


0 comments:

Post a Comment