Social

Saturday, March 11, 2017

Mabadiliko yaja CCM Dodoma




Dodoma. Mkutano Mkuu wa 12 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unafanyika Jumapili mjini Dodoma huku mabadiliko makubwa yakitarajiwa.
Mkutano huo mkuu unakwenda kupitia na kupitisha mapendekezo ya Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho uliofanyika Desemba mwaka jana jijini Dar es Salaam.
NEC iliyofanyika kwa mara ya kwanza chini ya mwenyekiti wake mpya Rais John Magufuli, ilipendekeza kupunguza idadi ya wajumbe wake kutoka 388 hadi 158 na wajumbe wa Kamati Kuu (CC) kutoka 34 hadi 24.

Si hayo tu, na idadi ya vikao imepunguzwa kwani NEC itakuwa na inakutana kila baada ya miezi sita tofauti na minne ya awali.
Ikiwa wajumbe wa Mkutano Mkuu watakubaliana na hoja hizo, ni wazi kuwa idadi ya wajumbe itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa, jambo linaloelezwa ni kubana matumizi pamoja na kutunza siri za vikao.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo katika taarifa yake amesema mkutano huo unafanyika kufuatia mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya chama ambayo yanasababisha muundo wenye mabadiliko na mfumo wa kiuongozi.
Mkutano huo wa siku moja utajadili na kupitisha marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012, pamoja na kanuni za chama hicho na jumuiya zake.
Kazi nyingine katika mkutano huo ni kupokea taarifa ya ratiba ya uchaguzi mkuu wa chama na jumuiya zake, utakaofanyika nchini kote mwaka huu.
Mkutano huo utatanguliwa na mikutano ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM na kufuatiwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)

0 comments:

Post a Comment