Dar es salaam. Kamati ya kuhamasisha timu ya Taifa ya vijana 'Serengeti Boys 'imeweka wazi mipango yao itakayotumika kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye fainali za Mataifa ya Afrika na hatimaye Kombe la Dunia kwa vijana nchini India.
Serengeti iko katika maandalizi kujiandaa na fainali hizo zitakazoanza Mei nchini Gabon.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Charles Hiraly amesema mchakato wa kuchangia timu upo wazi na si fedha tu zinazohitajika bali hata huduma mbalimbali za kijamii.
"Tumeyafikia tayari baadhi ya makampuni yameonyesha nia ya kutusaidia na tunaendelea kufanya mawasiliano na makampuni mengine" anasema Hilary.
Alisema hawahitaji fedha tu bali vitu vingine mbalimbali mfano chakula, tiketi za ndege zitakazokuwa msaada kwa timu hiyo inayojiandaa na fainali za Afrika zitakazoanza Mei .
0 comments:
Post a Comment