Social

Thursday, March 16, 2017

Hakimu matatani akidaiwa kuomba rushwa


Tabora.  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa, inamhoji hakimu wa mahakama ya mwanzo kwa tuhuma za kuomba rushwa kwa watu aliokuwa akisikiliza shauri lao.
Kamanda wa Takukuru mkoa wa Tabora, Fidelis Kalungura amesema ofisi yake inaendelea na uchunguzi wa tuhuma dhidi ya hakimu huyo na endapo ikithibitika atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani.
Kalungura amebainisha kuwa hakimu huyo alikamatwa hivi karibuni na kwamba uchunguzi dhidi yake unaendelea.
Amesema hakimu huyo anatuhumiwa kuomba kati ya Sh250, 000 na Sh500, 000 ili aweze kutoa maamuzi yenye upendeleo.

0 comments:

Post a Comment