Social

Monday, March 6, 2017

DPP aondoa shtaka la Lissu, akamatwa tena





Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondoa shtaka la uchochezi lililokuwa linamkabilia Mbunge wa Singida Mshariki, Tundu Lissu.
Lissu alikuwa akishtakiwa kwa kutoa maneo ya uchochezi Januari 11 mwaka huu akiwa Kibunju Maungoni B wakati wa kampeni za uchaguzi wa jimbo la Dimani.
Hata hivyo muda mfupi baada ya shtaka kuondolewa mahakamani, Lissu alikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene leo muda mfupi baada ya Lissu kuachia imeeleza kuwa mbunge huyo alikamatwa na hadi sasa haijaelezwa amekamatwa kwa sababu gani.

0 comments:

Post a Comment