Social

Thursday, March 23, 2017

DC Madusa, washtakiwa watoana jasho mahakamani


Chunya. Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa juzi alitumia saa mbili mahakamani akitoa ushahidi kwenye kesi ya jinai huku mshtakiwa akimhoji ni kwa nini kituo cha kupigia kura kiliwekwa eneo la hifadhi ambako wanatakiwa kuondoka.
Washtakiwa hao Rocket Kija (44) na Juke Japhet wakazi wa Kata ya Kambikatoto, wanadaiwa kuhamasisha watu wasitii amri ya mkuu huyo wa wilaya.
Walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Chunya, Oktoba mwaka jana wakikabiliwa na kosa la kuhamasisha wananchi wasitii agizo la mkuu huyo wa wilaya lililowataka kuondoka eneo la Hifadhi la Sipa.
Akitoa ushahidi mahakamani hapo, Madusa alidai kwa mara ya kwanza alifika eneo la Sipa Agosti 18, mwaka jana baada ya kupata taarifa kuwa kuna wananchi wameanzisha kijiji ndani ya hifadhi.
Alisema alifanya mkutano uliolenga kuwaelimisha kwamba eneo hilo ni la hifadhi na wanatakiwa kuondoka na kuacha maeneo yote ya kijiji hicho ikiwa ni pamoja na vitongoji walivyovianzisha vya Kwaikulu, Madaso, Chamaondo, Majiweni, Mbuzi na Sipa ambako alidai kuna wanyamapori na ni msitu wa hifadhi.
Madusa alidai tamko la kuwataka waondoke kwa hiari alilitoa Septemba 16, 2016 baada ya kumaliza mkutano na kwamba, alitoa siku 14 na kuwaagiza viongozi wa vitongoji na vijiji kusimamia suala hilo.

0 comments:

Post a Comment