Social

Thursday, March 16, 2017

Boko haram lashambulia mji wa Magumeri Nigeria

Wapiganaji wa kundi la Boko haram wanadaiwa kutekeleza mashambulio kiholela
Image capti
Ripoti kutoka kaskazini mwa Nigeria, zasema kuwa watu waliokuwa na silaha na wanaoaminika kuwa wanamgambo wa kundi la kiislamu la Boko Haram, wametekeleza shambulio katika mji wa Magumeri.
Duru zasema kuwa waliwashambulia raia kiholela huku wakiteketeza majumba yao.
Kuna ripoti inayosema kuwa, moshi mkubwa unaonekana ukifuka kutoka eneo ambalo kituo cha polisi kiko mjini humo.
Jeshi la Nigeria halijatoa taarifa zozote kuhusiana na shambulio hilo.
Awali wanawake wanne walipuaji wa kujitolea kufa walijilipua katika mji ulioko karibu wa Maiduguri, na kusababisha vifo vya watu wawili.
Jimbo la Borno, limekumbwa na maafa mabaya na uhasama kati ya majeshi ya serikali na Boko Haram kwa muda wa miaka minane sasa.

0 comments:

Post a Comment