Social

Monday, April 10, 2017

Mamba wala watu wageuka tishio


Kitendo cha wakazi wanne wa kata za Kazunzu na Bulyaheke wilayani Sengerema, kuliwa na mamba kimesababisha ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kutoa kibali cha kuwaua.
Wakazi hao wameingiwa hofu kutokana na uwapo wa mamba ambao wamesababisha vifo hivyo.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kazunzu, Chuma Sengerema na mwenzake wa Bulyaheke, Mussa Mwilomba kwa nyakati tofauti walisema vifo hivyo vilitokea kati ya Agosti mwaka jana na Aprili mosi.
Waliouawa ni John Thomas (36), aliyefariki dunia Oktoba 21, 2016 na Juma Abdallah aliyeuawa Agosti 24 mwaka jana. Wengine ni Diana Majani aliyeuawa Machi 13 ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la pil Shule ya Msingi Soswa.  Pia, Kadada Benjamin aliyeuawa Aprili mosi.
Katika mlolongo wa matukio hayo, mkazi mwingine aliyetajwa kuwa Stella Bano alinusurika kifo, baada ya kujeruhiwa alipokamatwa na mamba alipokuwa akifua kando ya Ziwa Victoria.

0 comments:

Post a Comment