Social

Monday, April 10, 2017

Dk Magufuli ateua kamati ya pili kuchunguza mchanga wa madini


Dar es Salaam. Rais John Magufuli ameteua wajumbe nane wa kamati maalum ya pili itakayofanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Taarifa iliyotolewa leo asubuhi na  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imewataja wajumbe hao kuwa ni Profesa Nehemiah Osoro, Profesa Longinus Rutasitara, Dk Oswald Mashindano na Gabriel Malata.
Wengine ni Casmir Kyuki, Butamo Philip, Usaje Usibwe na Andrew Massawe.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa wajumbe hao wataapishwa kesho Aprili 11 saa 3:00 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment