KIKOSI cha Yanga leo kitakuwa na kibarua kipevu kwa kuwakabili mabingwa wa Zambia Zanazo, katika mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hicho ni kibarua kigumu kwa kocha wa Yanga George Lwandamina, kutokana na uwezo waliokuwa nao Zanaco na kikosi chake ambacho kwasasa kina wachezaji wengi majeruhi.
Nyota ambao wana hati hati ya kucheza mechi ya leo dhidi ya Zanaco ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Juma Abduli, licha ya baadhi yao kuonekana mazoezini wakijiandaa na mchezo huo.
Kocha Lwandamina licha ya kuifahamu vizuri Zanaco, lakini amekiri kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu, na kuwa raia wa Zambia au kuifahamu vizuri timu hiyo siyo kigezo cha Yanga kushinda ispokuwa kinachohitajika ni wachezaji kucheza kwa kujituma ili kupata ushindi.
"Ni kweli nawafamu vizuri Zanaco kwasababu walikuwa wapinzani wangu wakubwa wakati naifundisha Zesco, lakini mimi kuwa Mzambia au kuwafahamu vizuri siyo kigezo cha kuwapa matumaini mashabiki wa Yanga kuwa, tunaweza kushinda kwani mpira wa siku hizi unamabadiliko makubwa kitu cha msingi ni wachezaji kucheza kwa kujituma kuipigania timu yao kupata ushindi," alisema Lwandamina.
Kocha huyo alisema mandalizi yao yamekamilika kwa ajili ya mchezo huo na wanatarajia kucheza kwa kushambulia, ili kuweza kupata ushindi, ambao utawaweka sehemu salama kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki moja nchini Zambia.
Zanaco FC ya Zambia waliotua Dar es Salaam, tangu juzi jioni kwa ajili ya pambano hilo, ambalo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi moja kwa moja huku atakayetolewa atatua katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha wa Zanaco Mumamba Numba alisema timu yake iko tayari kwaajili ya kuwakabili Yanga leo na hana chochote cha kuahidi zaidi ya kuacha dakika 90, za kwanza kuamua mshindi atakayefuzu hatua ya makundi.
Numba alisema anamfahamu vizuri kocha wa Yanga Lwandamina, kwani waliwahi kufanyakazi pamoja Zanaco, na wamekuja Tanzania wakiwa wanaijua vizuri Yanga na hawatarajii kuona mabadiliko kwa timu hiyo kwasababu wanazijua falsafa za kocha wao.
"Nimchezo rahisi kwetu licha ya kucheza ugenini na timu kubwa Tanzania, na hilo linatokana na kuwajua vizuri Yanga pamoja na uwezo wa wachezaji wake wote wakigeni na hata wazawa tunajua kuna Justine Zullu na Obrey Chirwa ni vijana wetu nawajua vizuri uwezo wao sidhani kama watakuwa na kitu kipya ila tuache dakika 90 zitaongea,"alisema Numba.
Numba alisema katika mchezo wa kesho watawakosa wachezaji wawili muhimu kwenye kikosi chao, ambao ni Fashion Sakala na kipa Mangani Banda, ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia ya vijana Young Chipolopolo, lakini hana hofu kwasababu wapo wachezaji wa kuziba nafasi zao.
Yanga wanaingia kwenye hatua hiyo baada ya kuitoa Ngaya Club de Mde ya Comoro kwa jumla ya mabao 6-2, wakati Zanaco iliitoa APR ya Rwanda kwa bao 1-0, ililoshinda Kigali kufuatia suluhu Lusaka, Zambia.
0 comments:
Post a Comment