Social

Friday, March 10, 2017

Waziri Ummy awashukia waajiri sekta binafsi


Singida. Waziri   wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  amewaonya waajiri wa sekta binafsi kuacha mara moja tabia ya kufukuza kazi wafanyakazi  wanapopata ujauzito na kuomba likizo kwenda kujifungua.
Pia, Waziri huyo amesema wanawake walioajiriwa katika sekta zote wana haki kisheria ya kupata likizo baada ya kujifungua.
Mwalimu amesema wapo baadhi ya waajiri wa sekta binafsi   mfanyakazi   wake akipata mimba, linakuwa  kosa la kumfukuzisha kazi mhusika.
"Tabia hii haikubaliki kabisa. Hatutakubali, tutamchukulia hatua kali mwajiri yoyote wa sekta binafsi, atakayebainika amefukuza  mfanyakazi, kisa amebeba mimba,"amesema Mwalimu.

0 comments:

Post a Comment