NAHODHA wa Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba amesema wanakwenda Gabon kupambana na lazima kieleweke. "Tunakwenda kuwakilisha nchi, hili ni jukumu kubwa kwetu lakini ni fursa pia kuonekana kwa kuwa michuano hiyo itakuwa ikifuatiliwa na mawakala mbalimbali."
Straika Yohana Mkomola alisema: "Kazi yetu ni kucheza, ila tunapoona watu wengine wanatuhamasisha inatutia moyo, kumbe hatuko peke yetu, lazima tupambane kwa kujiamini japo michuano hiyo ni migumu."
Serengeti wanaendelea kupiga tizi la mwishomwisho jijini Dar es Salaam kabla ya kusepa zao Kagera kucheza mechi maalumu, huku Kocha wake, Bakari Shime akitamba kuwa vijana wameiva hadi wanampa raha.
Timu hiyo inajiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wa U-17 na ikitoka Kagera itakwea mwewe kuelekea Morocco mapema mwezi ujao kuweka kambi ya mwezi mzima.
Timu hiyo itatua mjini Bukoba, Kagera kucheza mechi za kujipima nguvu dhidi ya Rwanda, Burundi na Uganda kisha itarudi Dar kufungasha virago kabla ya kusepa Aprili 4.
"Hii inanipa faraja kuwa tunaweza kufanya vizuri, tukishacheza mechi za majaribio, nitapata picha halisi ya tulipofikia," alisema Kocha Bakar Shime.
0 comments:
Post a Comment